Mhoji: Naam, leo ni Siku ya Ndimi Asilia Duniani, siku ambayo imetengwa na Umoja wa Mataifa ili kuhamasisha lugha mbalimbali duniani kote. Watu wengi barani Afrika wanaungumza zaidi ya lugha moja, lakini bado wanasalia kupenda lugha zao za asili. Umoja wa Mataifa unasema lugha nyingi duniani zinapotea kutokana na utandawazi, takribani nusu ya lugha zote 6,000 duniani ziko hatarini kupotea, lakini hata hivyo barani Afrika lugha moja Kiswahili, imejipenyeza na kupata umarufu sio tu ndani ya bara mbali hata nje. Mzungumzaji 1: Polisi [isiyoeleweka 00:00:28] huyu atafanya nini nitakapokuwa mbali. Mhoji: Wanafunzi wakisoma Kiswahili hapa London. Mzungumzaji 2: [Isiyosikika 00:00:36] What is dhamira? Mhoji: Hili ni somo maarufu sana katika chuo hiki ambapo wanafunzi kadhaa humaliza kila mwaka wakizungumza lugha hii kwa ufasaha. Mwanafunzi 1: Natoka Marekani nilijifunza Kiswahili nilipoenda Tanzania miaka mitatu iliyopita, nilikaa Mwanza kwa miaka miwili na nusu nikijifun...