Mhoji: Naam, leo ni Siku ya Ndimi Asilia Duniani, siku ambayo imetengwa na Umoja wa Mataifa ili kuhamasisha lugha mbalimbali duniani kote. Watu wengi barani Afrika wanaungumza zaidi ya lugha moja, lakini bado wanasalia kupenda lugha zao za asili. Umoja wa Mataifa unasema lugha nyingi duniani zinapotea kutokana na utandawazi, takribani nusu ya lugha zote 6,000 duniani ziko hatarini kupotea, lakini hata hivyo barani Afrika lugha moja Kiswahili, imejipenyeza na kupata umarufu sio tu ndani ya bara mbali hata nje.
Mzungumzaji
1: Polisi [isiyoeleweka 00:00:28] huyu atafanya
nini nitakapokuwa mbali.
Mhoji: Wanafunzi wakisoma Kiswahili hapa London.
Mzungumzaji
2: [Isiyosikika 00:00:36] What is
dhamira?
Mhoji: Hili ni somo maarufu sana katika chuo hiki ambapo
wanafunzi kadhaa humaliza kila mwaka wakizungumza lugha hii kwa ufasaha.
Mwanafunzi
1: Natoka Marekani nilijifunza Kiswahili nilipoenda
Tanzania miaka mitatu iliyopita, nilikaa Mwanza kwa miaka miwili na nusu nikijifunza
Kiswahili kule. Nikaanza kusoma hapa SOAS nanilitaka kuendelea na Kiswahili changu
ili kukiboresha kukitumia baadae kikazi.
Moe: Mimi jina langu ni Moe, ninatoka Japani sababu ya
kusoma Kiswahili yangu ni, kwanza, nilivutiwa na utamaduni ya kiafrika sana, kama
muziki na ngoma.
Jessica: Ninaitwa Jessica na ninatoka Ureno lakini wazazi
wangu wanatoka visiwa vya Cape Verde, na nisoma Kiswahili hapa SOAS kwa sababu
nafikiri kwamba Kiswahili ni lugha muhimu sana katika Afrika, na nina mpango
labda kufanya kazi katika Afrika ya Mashariki.
Greti: Ninaitwa Greti ninatoka Hungaria katika Ulaya
Mashariki. Na nilichagua kusoma Swahili
kwa sababu ni lugha kubwa zaidi katika Afrika.
Mhoji: Licha ya kuwa kuna lugha nyingi katika mataifa 54 ya
Afrika, Kiswahili kinavutia kwa sababu ya historia yake pana na nafasi yake, kama
lugha inayozungumzwa na wengi barani Afrika.
Mzungumzaji
3: Kwa imani pake.
Mhoji: Na kimataifa ilipata umamarufu mkubwa kutokana wimbo
na msemo wa hakuna matata. Msemo huu ambao umeekwa hati miliki na
kampuni ya Disney ya Marekani, umezua mtafaruku mkubwa kwa wazungumzaji wa
Kiswahili.
Mzungumzaji
4: Hili swala la kwamba hakuna matata huchukuliwa
kama alama ya biashara, mimi nafikiri si sahihi, kwa sababu, ingawa si
Kiswahili fasaha lakini ni maneno ya Kiswahili kwa hivyo unapoyachukua ni kama unachukua
lugha ya mtu utamaduni wa mtu unachukua utu wa mtu, sasa kama leo umechukua maneno yake kesho
utachukua nini?
Mhoji: Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 100
Afrika Mashariki na Kati na pia ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika na
kuna majadiliano ya kutaka kuifanya lugha hii kuzungumzwa na Waafrika wote.
Afrika Kusini hivi karibuni imeingiza Kiswahili kwenye mitaala yake.
Mzungumzaji
5: [lugha ya kiingereza] I go to conferences with fellow sisters from Africa -
-
Mkalimani:
Huwa na kwenda kwenye mikutano, na hukutana na watu
kutoka Afrika wakizungumza Kifaransa, Kiingereza na hakuna kinachotuunganisha
kama waafrika, kwa hio watoto wetu wanahitaji kitu ambacho nicha Kiafrika na
chenye kutuunganisha, na ni lugha ya Kiswahili.
Mzungumzaji
6: -- which is Kiswahili?
Mhoji: Wakati kuna wasiwasi kuwa mambo kama utandawazi
yanaadhili lugha nyingi duniani, Kiswahili kinaonekana kuchana mbuga katika kuunganisha
Bara la Afrika na pengine kuwa lugha ya Afrika.
[Mwisho
wa Sauti]
Would You Like Extra Training
ReplyDeleteYes
DeleteGreat connecting with you, you can create an Account with Ajira Digital for an exquisite training
ReplyDelete